Tuesday, April 23, 2013

Kikwete:Baadhi ya viongozi wa Afrika wanatumiwa na mataifa ya nje

 


Rais wa Tanzania, Jakaya Kikwete
Rais wa Tanzania, Dakt. Jakaya Mrisho Kikwete
 
nchini Tanzania Jumatatu ambapo suala la migogoro katika baadhi ya nchi za Afrika limejadiliwa.

Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kufungua mkutano huo wa AU Rais wa Tanzania Jakaya Kikwete alitoa tahadhari kwa baadhi ya viongozi barani Afrika  ambao amedai wanatumiwa na watu wa mataifa ya nje kuchochea migogoro katika bara hili

Bila kutaja majina yao Rais Kikwete alisema zama hizo za kutumiwa zimeanza kutoka wakati wa ukoloni mpaka hivi sasa.

Rais Kikwete alielezea chanzo cha migogoro barani Afrika ni kwamba ukoloni uliokuwa unawagawa waafrika ili uwatawale na pia mipaka ambayo mingi iliwekwa kwa maslahi ya watawala.

Aidha Rais Kikwete, alisifia juhudi za Umoja wa Afrika  kwa kushirikiana na vyombo vyake  katika kufanikisha kutatua matatizo yanayozikabili nchi mbalimbali barani humo ambapo alisema kwa sasa migogogoro mingi imepungua ikiwemo mgogoro wa hivi sasa nchini Madagascar.

Mkutano huo wa 368 wa baraza la amani na usalama la AU unafanyika kwa mara ya kwanza nchini Tanzania na  umeongozwa na Waziri wa Mambo ya Nje wa Tanzania Bernard Membe na kuhudhuriwa pia na rais mstaafu wa Msumbiji na mpatanishi mkuu wa mgogoro wa Madagascar Joachim Chisano.

No comments:

Post a Comment