Thursday, April 25, 2013

Generali wa Brazil kuongoza kikosi DRC

 
 
Umoja wa Mataifa umemteua Generali mmoja raia wa Brazil ambaye anasifika kwa kudhibiti mtaa mmoja wa mabanda nchini Haiti kutokana
na vurugu kuweza kuwaongoza walinda amani wa Umoja wa Mataifa katika Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Generali Carlos Alberto dos Santos Cruz ataongoza kikosi cha wanajeshi 20,000, ikiwemo kikosi kipya cha wanajeshi kitakachopambana na waasi mashariki mwa nchi.

Generali Santos Cruz, aliambia BBC kuwa wanajeshi wake, watafunzwa namna watakavyo pambana na waasi bila kuwajeruhi raia na kuharibu mali nchini Congo.

"Eneo tete zaidi siku hizi ni Mashariki mwa nchi,'' Cruz alimbia BBC
"niko tayari kukabiliana, na hali ngumu zaidi. Lengo kuu ni kuwaondolea hali ngumu wanayokabiliana nayo watu wa Congo.''
Generali Santos Cruz ataongoza kikosi cha wanajeshi 2,500, wakiwa na jukumu la kuwapokonya silaha waasi pamoja na kuwarejesha katika maisha ya kiraia Mashariki mwa DR Congo.''

Kikosi cha walinda amani cha Umoja wa mataifa,kilichoko Congo kimekosolewa sana kwa kukosa kumaliza vita, vya miongo miwili.
Wanajeshi kutoka Tanzania, Malawi, Msumbiji na Afrika Kusini ndio walio wengi katika kikosi hicho na wataanza kazi yao mwezi Julai.

Generali Santos Cruz ni kamanda mstaafu, wa kikosi kilichowahi kutumwa nchini Haiti, na anasifiwa kwa kupambana vikali na magenge ya majambazi nchini Humo mwaka 2007

No comments:

Post a Comment