Korea ya Kaskazini yazidisha nguvu za kijeshi.
Katibu mkuu wa Umoja wa mataifa
Ban Ki moon ameitaka Korea ya kaskazini kupunguza makali yake kwa mzozo
unaotokkota wa kinuklia akisema kuwa umeanza kuvuka mpaka.
Bwana Ban amesema kuwa anahuzunishwa na namna ugomvi huo unavyotishia maisha ya wananchi wa kawaida.
Akizungumzia
vitisho vya karibuni sana vya Korea Kaskazini kwa Korea Kusini na
Marekani, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Ban Ki Moon alisema kuwa hali
hiyo imekuwa ya kustajabisha na kusikitisha.
Alisema kuwa Korea Kaskazini imezidisha vitisho vyake na akaonya kuwa cho chote kinaweza kuzusha kitendo cha kusikitisha.
Bwana Ban aliyekuwa wakati mmoja Waziri wa
Mashauri ya Kigeni wa Umoja wa Mataifa, alitoa wito kwa viongozi wa
Korea kaskazini kubadili mwenendo wao.
Awali msemaji wa Wizara ya mashauri ya Kigeni wa
Urusi alisema kuwa uamuzi wa Korea Kaskazini kuendeleza mpango wake wa
kuimarisha uwezo wake wa zana za kinukilia unavuruga mipango ya
kuanzisha upya mashauriano yanayohusu mataifa sita ya kupatanisha Korea
Kusini na Kaskazini.
Mataifa yanayokusudiwa kushiriki katika mashauriano hayo ni Korea Kusini, Korea Kaskazini, Uchina, Urusi, Japan na Marekani.
Msemaji huyo alieleza kwamba juhudi zo zote za kupuuza maazimio ya Umoja wa Mataifa hazikubaliki.
No comments:
Post a Comment