Ufaransa inasema inaweza
kuthibitisha kifo cha Abou Zeid, mmoja kati ya makamanda waandamizi wa
al Qaeda katika Afrika Magharibi.
Inaarifiwa kuwa aliuliwa na wanajeshi wa Ufaransa kaskazini mwa Mali mwezi uliopita. Ofisi ya rais wa Ufaransa inasema ukaguzi wa DNA umewezesha kumgundua rasmi Abou Zeid. Aliongeza kusema kuwa kifo cha Abou Zeid ni hatua muhimu katika vita dhidi ya ugaidi katika kanda ya Sahel. Wanajeshi wa Ufaransa na wa nchi za Afrika
wamekuwa wakipigana dhidi ya wapiganaji wa Kiislamu nchini Mali tangu
mwezi wa Januari.
No comments:
Post a Comment