Kazi yaendelea Vatican.
Siku yake ya kwanza ofisini kama
Papa mtakatifu wa kanisa Katoliki, Papa Francis 1 tayari anaanza
kazi.
Papa anatarajiwa kuwateua wafanyikazi wakuu watakaohudumu katika Vatican
chini ya uongozi wake. Ameanza siku yake kwa maombi ya kibinafsi katika
hekalu ya mtakatifu Maria Maggiore mjini Rome.
Baadaye Papa atafanya misa ya sherehe katika kanisa la Sistine.
Mwandishi wa BBC anasema kuwa uteuzi atakaofanya
Papa Francis, utatizamiwa kama ishara ya mageuzi katika uongozi
uliozongwa na kashfa nyingi na pia utaonyesha mwelekeo anaonuia kuchukua
kwa kanisa hilo.
Papa Francis 1.
Baadaye wikendi ijayo, Papa mpya anatarajiwa kukutana na vyombo vya habari vya dunia katika mkutano maalum.
Na Jumapili, ataongoza misa yake ya kwanza kama
papa. Hata hivyo yeye mwenyewe atatawazwa rasmi kuwa Papa Francis 1,
siku ya Jumanne.
No comments:
Post a Comment