Monday, March 18, 2013

Odinga afikisha malalamiko mahakamani

 

Bwana Raila Odinga
 
Polisi mjini Nairobi, Kenya, wamefyatua moshi wa kutoa machozi kuwatawanya mamia ya wafuasi wa Waziri Mkuu Raila Odinga, nje ya mahakama makuu.
Mawakili wa Bwana Odinga waliwasilisha kesi mahakamani kupinga matokeo ya uchaguzi mkuu wa mapema mwezi huu, ambapo Bwana Odinga alishindwa kwa kura elfu chache na Bwana Uhuru Kenyatta.

Hapo awali Bwana Odinga aliwasihi wafuasi wake wasijihusishe na vurugu.
Mawakili wa Bwana Odinga wamekwenda mahakamani wakidai kuwa kumepita udanganyifu kwenye uchaguzi.

No comments:

Post a Comment