Mahakama kuu ya mjini
Mogadishu Somalia imemwaachilia huru mwandishi wa habari ambaye
alifungwa kwa sababu ya kumhoji mwanamke aliyesema amebakwa.
Katika kesi iliyolalamikiwa kimataifa, mwandishi
huyo, Abdilaziz Abdinuur, awali alipewa hukumu ya kifungo cha mwaka
mmoja kwa kumhoji mwanamke ambaye alisema alibakwa na wanajeshi wa
serikali.Mwanamke huyo piya alihukumiwa kifungo cha mwaka mmoja lakini kesi yake ilifutwa kwenye rufaa awali mwezi huu.
Jaji wa mahakama makuu - Aidid Abdulahi Ilkahanaf - alisema mashtaka yote dhidi ya mwandishi huyo wa habari sasa yamefutwa.
No comments:
Post a Comment