Wakuu wa jeshi nchini Mali
wanasema mshambuliaji aliyejitolea mhanga ameuwawa, akijaribu kujiripua
kwenye kituo cha ukaguzi mjini Timbuktu, kaskazini mwa nchi.
Mwanajeshi mmoja alijeruhiwa.
Mwandishi wa BBC nchini Mali anasema tangu wakati huo risasi zimekuwa zikifyatuliwa magharibi mwa mji huo.
Timbuktu imekuwa mikononi mwa wapiganaji wa
Kiislamu kwa miezi kumi hadi walipofurushwa na wanajeshi wa Ufaransa
awali mwezi March.
Wanajeshi wa Ufaransa na Afrika wanasema
wamefanikiwa kuzuwia uvamizi wa eneo la kaskazini mwa Mali uliofanywa na
wapiganaji wa Kiislamu.
Ufaransa itaanza kuondosha wanajeshi wake mwezi
Aprili lakini baadhi yao watabaki, pengine watajumuika na kikosi cha
Umoja wa Mataifa.
No comments:
Post a Comment