Sunday, March 24, 2013

Mambo 30 yanayokuonyesha umri umekwenda

Kutoka kwa msomaji mwenzetu: Linda Mtengule
Embu angalieni, je ni sawa haya mambo yanaonesha kuwa umri umekwenda?
1. Huna muda wa kushinda na mpenzi wako kutwa nzima mkipiga stori za mapenzi.

2. Ukihitaji kufanya mapenzi mahali unakokufikiria ni kitandani.

3. Unaanza kujaza friji lako kwa vyakula zaidi kuliko pombe.

4. Muziki unaoupenda unausikia ukiwa kwenye lifti ama kwenye gari lako ukienda na kutoka kazini.

5. Saa 11 alfajiri ndiyo muda unaoamka, na siyo muda tena unaorudi kulala.


6. Unatazama taarifa ya habari hadi utabiri wa hali ya hewa.

7. Rafiki zako wanakualika zaidi kwenye vikao vya harusi kuliko mtoko wa kwenda Maisha Club.

8. Ukienda dukani kununua kitu unakuwa na juhudi sana ya kuomba upunguziwe bei.

9. Idadi ya t-shirt na jeans inapungua kwa kasi kwenye kabati lako la nguo.

10.Wewe ndiyo unayekumbuka kuwapigia simu Polisi endapo mtaani kwenu kuna vijana wavuta bangi wanaowasumbua.

11. Ndugu zako watu wazima wanajisikia kawaida tu kufanya utani wa kiutu uzima mbele yako.

12. Hukumbuki tena Azam Ice Cream na Samaki Samaki wanafunga saa ngapi.

13. Timu yako ya mpira ikifungwa hutaki tena kutaniwa na watu.

14. Wanyama uwapendao kama mbwa na paka unawaandalia chakula kwa kanuni za kisayansi badala ya kuwalisha makombo.

15. Ukilala kwenye kochi unaamka mgongo unakuuma sana.

16. Unaithamini sana ratiba yako ya kulala.

17. Ukiwa nyumbani unaanza kutumia muda wako wa ziada kulimalima bustani ya maua ama mbogamboga badala ya kutazama filamu na kuzurura.

18. Kila kitu kikinunuliwa nyumbani jambo la kwanza unalouliza, "Umenunua sh. ngapi?".

19. Unakwenda duka la madawa kununua Ibuprofen na Antacid, siyo kondomu tena wala kipima mimba.

20. Unaanza kununua magazeti ya Mwananchi, The Guardian, Daily News, Citizen na Nipashe badala ya Uwazi, Ijumaa, Kiu na Amani.

21. Unapata kifungua kinywa kwa wakati.

22. Ukiwa baa unanunua bia unazohitaji wewe badala ya kusema "zungusha kama tulivyo".

23. Asilimia 90 ya muda unaoutumia kwenye kompyuta yako unautumia kufanya kazi badala ya kuchati.

24. Ukijisikia hamu ya kunywa kilevi unaanza kunywea nyumbani ili kupunguza gharama kabla hujaenda baa.

25. Ukimwona rafiki yako ana ujauzito unampongeza sana badala ya kumwuliza, "imekuwaje tena?".

26. Ukienda kutembea mahali unaulizia bei za viwanja.

27. Hupendi tena kuwaazimisha marafiki zako magari yako.

28. Ukiwa na rafiki zako unapenda kujadiliana nao kuhusiana na mfumuko wa bei, na mfumo mbovu wa utawala.

29. Ukiwa unakula chakula unakuwa mkali ikitokea chakula kimewekwa mafuta mengi ama chumvi nyingi.

30. Kwa wanawake utaanza kuona vijana wanakukimbia na kwa wanaume utaanza kuona vibinti vinakupapatikia sana .

Ukiona una robo ya sifa hizi 30 basi huhitaji kupigiwa kengele kukumbushwa kuwa umri ushayoyoma.

No comments:

Post a Comment